WABABE NANE NDANI 16 BORA, WANASUBIRIWA NANE WENGINE KUTIFUANA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

 Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) imefikia tamati hapo Jana Januari 28, 2026 kwenye hatua ligi iliyojumuisha Jumla ya michezo nane kwa Kila timu , huku timu nane zilizo ongoza kwa alama zikikata tiketi ya moja kwa moja kwenda hatua ya 16 Bora, na timu nane nyingine zikilazimika kusubiri hatima yao kupitia michezo ya mtoano (play-offs).

Kwa mujibu wa msimamo wa mwisho, vigogo nane vilivyoonyesha ubabe mapema na kujihakikishia nafasi ya moja kwa moja ni pamoja na Arsenal, Bayern Munich, Liverpool, Tottenham, Barcelona, Chelsea, Sporting CP na Manchester City.

Katika orodha ya timu nane zilizofuzu nne, zimetokea nchini England ikiwa ni nusu ya timu zilizofuzu Moja Kwa Moja wakionyesha hali ya kulitawala soka la ulaya .

Katika hatua nyingine mabingwa wa kihistoria wa kombe hilo Real Madrid watalazimika kucheza mtoano baada ya kushindwa kupata matokeo mbele ya Benfica kufuatia kichapo Cha 4-2, Madrid walihitaji angalau alama Moja kufuzu Moja kwa Moja lakini ilishindikana.

Kwa sasa, mashindano yanaingia katika sura mpya yenye msisimko mkubwa, ambapo timu zilizopo mtoano zitapambana vikali kuungana na wababe hao nane tayari waliopo 16 Bora.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments