WABABE NANE AFRIKA KUTIFUANA JANUARI 9 NA10 KUISAKA NUSU FAINALI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yameingia hatua ya robo fainali itakayochezwa nchini Morocco kuanzia Januari 9 na 10, 2025, huku miamba ya soka barani Afrika ikitarajiwa kupambana vikali kusaka tiketi ya nusu fainali.

Kwa mujibu wa ratiba rasmi , Januari 9kutakuwa na mi hezo miwili ambapo saa 1:00 usiku, Mali itavaana na Senegal katika pambano la Afrika Magharibi linalotarajiwa kuwa na ushindani mkali, kila upande ukiwa na lengo la kuandika historia, Baadaye saa 4:00 usiku, wenyeji Morocco watashuka dimbani dhidi ya Cameroon.

Ratiba itaendelea Januari 10 ambapo kutakuwa na michezo miwili mikubwa ambapo Algeria itachuana na Nigeria kuanzia saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, katika pambano linalotarajiwa kuwa la kasi kutokana na historia na ubora wa vikosi vyote viwili, Usiku huo huo saa 4:00 usiku, Misri itakabiliana na Ivory Coast, mchezo unaokutanisha mabingwa wa zamani wa AFCON katika vita ya nguvu, mbinu na uzoefu.

Timu zinazopewa nafasi ya kuvuka hatua ya nusu fainali ni pamoja na Nigeria , Ivory coast, Senegal na Wenyeji Morocco, hii ni kwa mujibu wa wachambuzi huku utabiri ukizingatia uwezo wa vikosi ,ubora wa wachezaji na historia ya mashindano. je , timu tajwa ndizo zitakazo kata tiketi ? muda utaongea ambapo mbichi na mbivu vitaonekana.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments