Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Ligi Kuu ya England (EPL) imeendelea kutoa picha ya msimu wenye ushindani mkali baada ya wababe wengi kushindwa kuonja ushindi katika michezo iliyochezws wiki hii kwenye mzunguko wa 21hali iliyowapa fursa Arsenal kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama sita.
Katika mchezo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu , Arsenal walitoshana nguvu kwa sare ya 0-0 dhidi ya Liverpool , sare hiyo iliwatosha The Gunners kuendelea kulinda nafasi yao ya juu, wakionyesha uimara wa kikosi chao na nidhamu ya kiuchezaji, hasa upande wa ulinzi huku majogoo wakishinda kupiga hata shuti Moja langoni.
Mzunguko huu haukuwa wa neema kwa vigogo ambapo Chelsea waliendelea kuyumba baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Fulham, huku Tottenham wakipoteza kwa 3-2 dhidi ya Bournemouth huku Manchester United nao walilazimishwa sare ya 2-2 na Burnley, matokeo yaliyoongeza maswali juu ya uthabiti wao msimu huu.
Aston Villa walishindwa kutumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kutoka sare ya 0-0 dhidi ya Crystal Palace, wakati Manchester City wakikwama kwa sare ya 1-1 dhidi ya Brighton, matokeo yaliyowashusha katika mbio za kusaka kilele.
Kwa ujumla, mzunguko huu wa ligi umeonyesha wazi kuwa hakuna timu kubwa iliyofanikiwa kupata ushindi miongoni mwa Arsenal, Liverpool, Chelsea, Manchester United, Aston Villa wala Tottenham. Badala yake, sare na vipigo vimetawala, hali inayozidi kuipa Arsenal nafasi ya kupumua kileleni.
Kwa tofauti ya alama sita kileleni, Arsenal wanaendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa, huku wapinzani wao wakilazimika kujipanga upya haraka iwapo wanataka kubaki kwenye mbio za taji la EPL msimu huu.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
.jpeg)
Post a Comment