Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Manchester United imeonyesha sura mpya ya matumaini na kujiamini baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Manchester City, katika Manchester Dabi iliyochezwa jana kwenye uwanja wa Old Trafford.
Chini ya kocha mpya wa muda, Michael Carrick, United imeonekana kuwa timu tofauti kabisa yenye nidhamu, kasi na mpangilio mzuri wa kiufundi, Ushindi huo haukuwa wa bahati mbaya, bali ulikuwa ni matokeo ya mipango sahihi, morali ya juu ya wachezaji na ari mpya iliyorejea ndani ya kikosi cha Mashetani Wekundu.
United ilidhibiti mchezo kwa umakini mkubwa, ikicheza soka la kushambulia kwa tahadhari huku ikiziba vyema mianya ya City , Mabao mawili yaliyopatikana yalikuwa kielelezo cha kazi kubwa ya benchi la ufundi, pamoja na wachezaji waliojituma kwa hali ya juu, wakionesha kiu ya kurejesha heshima ya klabu hiyo kongwe.
Kwa upande wa Manchester City, kipigo hicho kimeibua maswali mazito kuhusu uimara wao katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England , City ilionekana kukosa makali tofauti na ilivyo zoeleka, huku safu yao ya ulinzi ikionekana kuyumba na washambuliaji wakishindwa kutumia nafasi walizopata.
Matokeo haya yanaacha mashaka kama City itaweza kuhimili presha ya ushindani mkali wa msimu huu, hasa wanapokutana na timu zinazocheza kwa nidhamu na kasi kama ilivyooneshwa na United , Kupoteza pointi muhimu katika dabi kama hii kunaweza kuwa pigo kubwa kwenye mbio za kunyakua taji.
Kwa Manchester United, huu ni ushindi unaotuma ujumbe mzito kwa wapinzani wao kwamba enzi mpya chini ya Michael Carrick zimeanza, na Old Trafford imeanza kurejesha hofu yake.
Ikiwa mwenendo huu utaendelea, basi United inaweza kuwa mshindani halisi katika hatua hizi za mwisho za msimu ikiwemo kusaka nafasi nne za juu, huku mashabiki wao wakianza kuamini tena katika “United Mpya” inayozaliwa upya.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment