UCL HAIJAISHA MPAKA IISHE, BENFICA NA MADRID USO KWA USO

HII HAPA DROO KAMILI HATUA YA MTOANO

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Droo hatua ya mtoano kuzitafuta timu nane zitakazo ungana na timu nane zilizokwisha fuzu kutinga 16 Bora mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya ( UEFA champions league) imefanyika January 30 , 2026 , huku timu zilizo salia kucheza hatua ya mtoano zikiwatambua wapinzani wao.

Kitu Cha kuvutia katika droo hiyo ni baada ya vilabu vya Real Madrid na Benfica kukutana kwenye hatua hiyo ya mtoano, ikumbukwe mchezo wa mwisho wa kukamilisha hatua ya ligi hiyo ilishuhudiwa Benfica akiibuka na ushindi wa 4-2 akiwa nyumbani matokeo yaliyo ifanya timu hiyo kuepuka kuondoka Moja kwa Moja huku Madrid wakishindwa kufuzu Moja kwa Moja kutokana na athari ya kipigo hicho.

Huu utakuwa ni mchezo wa kisasi na unatarajiwa kuwa mgumu na wenye ushindani kuanzia kwenye benchi la ufundi hadi uwanjani, Madrid ni mabingwa wa kihistoria kwenye kombe hili huku wakiwa na wachezaji imara kama Mbappe, vinicius na Bellingham lakini upande wa Benfica Wana kocha Jose Mourinho anae ifahamu vizuri Real Madrid hivyo upinzani unatarajiwa kuwa mkali.

Mchezo mwingine unatarajiwa kutengeza historia ni Newcastle United dhidi ya Quarabag ambapo kama Newcastle atafanikiwa kufuzu basi ataifanya ligi kuu nchini England kuingiza Jumla ya timu sita katika hatua hiyo ya 16 Bora baada ya Arsenal, Chelsea, Man City , Liverpool na Tottenham kufuzu Moja kwa Moja.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments