Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Chelsea imemtangaza rasmi Liam Rosenior kuwa kocha mpya wa timu hiyo, hatua inayomaliza sintofahamu ya muda kuhusu hatima ya benchi la ufundi la The Blues kufuatia kuachana na alie kuwa kocha wao Enzo Maresca baada ya mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha.
Rosenior, aliyekuwa akiinoa Strasbourg ya Ufaransa, amepewa dhamana ya kuirejesha Chelsea katika ushindani wa juu wa Ligi Kuu England na mashindano ya Ulaya, baada ya uongozi wa klabu hiyo kuridhishwa na falsafa yake ya soka la kushambulia, matumizi ya vijana pamoja na nidhamu ya kiufundi.
Uongozi wa Chelsea umeeleza kuwa uteuzi wa kocha huyo ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kujenga timu yenye mwelekeo mpya, inayozingatia soka la kisasa, maendeleo ya wachezaji vijana na ushindani wa kudumu.
Rosenior anatarajiwa kuanza majukumu yake mara moja, pamoja na benchi jipya la ufundi litakalojumuisha makocha wasaidizi walioteuliwa na klabu hiyo kwa kushirikiana naye.
Mashabiki wa Chelsea sasa wana matumaini mapya baada ya kipindi kigumu kilichojaa presha na matokeo yasiyo na uhakika, wakiamini kuwa ujio wa Rosenior unaweza kuwa mwanzo wa ukurasa mpya Stamford Bridge.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment