TETESI ZA USAJILI MSIMBAZI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Simba SC ipo mbioni kukamilisha usajili wa kipa mwingine wa kigeni kufuatia majeraha yanayomkumba kipa namba moja wa klabu hiyo Pin Pin Camara, jeraha ambalo limemuweka nje ya uwanja kwa muda na kuibua hitaji la dharura la kuongeza chaguo katika nafasi ya ulinda lango.

Kutokana na hali hiyo, Simba imeanza mchakato wa kutafuta kipa mbadala ili kuhakikisha kikosi kinaendelea kuwa imara kuelekea michezo ijayo ya ndani na ya kimataifa, huku Pin Pin Camara akiendelea na matibabu na anatarajia kutolewa nje ya mfumo wa wachezaji wa timu hiyo.

Sambamba na hilo, klabu hiyo imemtoa kiungo wake Mzamiru Yassin kwa mkopo kwenda klabu ya TRA United, hatua hiyo imelenga kumpa mchezaji huyo nafasi ya kupata muda zaidi wa kucheza baada ya kukosa dakika za kutosha ndani ya kikosi cha kwanza cha Simba.

Kwa mujibu wa taarifa, Mzamiru Yassin amebakiza takribani miezi sita katika mkataba wake na Simba SC ambao unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Katika hatua nyingine katika uboreshwashi wa kikosi baadhi ya wachezaji wa Simba wapo hatarini kuachwa Januari hii , wachezaji hai ni pamoja na Joshua Mutale, Steven Mukwala, Chamou Karaboue na Mligo.

Wachezaji wanaowindwa na klabu kuchukua nafasi hizo ni pamoja na Nickson Kibabage na Khadim Diaw ambao wanahusishwa kumwaga wino muda wowote.

Hatua hizi zinaonyesha Simba SC inaendelea kufanya marekebisho ya kimkakati ndani ya kikosi chake, huku ikilenga kudumisha ushindani na ubora katika mashindano yote inayoshiriki.

0767815473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments