BADO HATUA CHACHE JOHN BOSCO NCHINDO KUTUA MSIMBAZI

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Simba SC imepiga hatua kubwa katika usajili baada ya kufikia makubaliano ya awali na kiungo wa klabu ya Coton Sport ya Cameroon, John Bosco Nchindo, mwenye umri wa miaka 23.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya karibu na klabu hiyo yenye maskani yake Msimbazi, tayari wamekubaliana na upande wa mchezaji, huku kinachosubiriwa kwa sasa ikiwa ni kumalizana rasmi na uongozi wa Coton Sport ili dili hilo kukamilika.

John Bosco Nchindo ni mmoja wa viungo waliong'ara kwenye Ligi Kuu ya Cameroon msimu uliopita, kiasi cha kutwaa tuzo ya mchezaji bora ligi kuu ya Cameroon, ikiwa ni ishara ya kiwango chake bora na mchango mkubwa alioutoa kwa timu yake.

Endapo Simba SC watafikia makubaliano ya mwisho na Coton Sport, basi usajili huo utakamilika ndani ya muda mfupi na mchezaji huyo anatarajiwa kutua Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano ya ndani na kimataifa.

Ujio wa Nchindo utaongeza chachu kubwa katika safu ya kiungo ya Simba, ambayo imeonekana kuhitaji damu mpya kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya CAF Champions League.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments