TER STEGEN AAGA BARCELONA, AJIUNGA GIRONA KWA MKOPO.

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kipa wa FC Barcelona, Marc-Andre ter Stegen, ameshindwa kuzuia machozi alipokuwa anawaaga wachezaji wenzake na benchi la ufundi la klabu hiyo, baada ya kukamilisha uhamisho wa mkopo kwenda Girona hadi mwezi Juni.

Ter Stegen ameagana rasmi na kikosi cha Barcelona kwa msimu huu kupitia ujumbe wake wanwazi kwa mashabiki, marafiki na familia ya klabu hiyo, akieleza hisia zake nzito baada ya kuhitimisha safari yake ya muda mrefu ndani ya klabu aliyoiita “nyumbani”

Kipa huyo raia wa Ujerumani amesema Barcelona ni mahali alipokua siyo tu kama mchezaji bali pia kama nyumbani akishuhudia na kuishi nyakati nyingi zisizosahaulika katika maisha yake ya soka.

“Ninajisikia mwenye shukrani kubwa na fahari, Naipenda klabu hii, mji huu na eneo hili, Ni hisia ambazo hazitafifia kamwe, Msaada wenu kwa miaka yote umekuwa wa kipekee, asanteni ” alisema.

Ter Stegen pia alitoa shukrani maalum kwa wachezaji wenzake akisisitiza mshikamano, heshima, furaha na mapambano waliyopitia kwa pamoja, huku akibainisha fahari ya kuvaa kitambaa cha unahodha wa Barcelona kama heshima kubwa atakayobeba maisha yake yote.

Sasa safari mpya inaanza kwa kipa huyo ndani ya ardhi ya Catalonia akiwa na Girona, huku akieleza matumaini makubwa akiwatakia kila la heri FC Barcelona katika safari yao siku zijazo.

0767915474,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments