TANZIA: PETER MANYIKA AFARIKI DUNIA

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Soka la Tanzania na Klabu ya Young Africans wamekumbwa na majonzi mazito baada ya golikipa wa zamani wa klabu hiyo na mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ( Taifa stars), Peter Manyika, kufariki dunia alfajiri ya leo Januari 26, 2026.

Manyika amefariki akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya St. Monica, Dar es Salaam, baada ya kusumbuliwa na maradhi ya muda mrefu, Kifo chake kimeacha pengo kubwa katika historia ya soka la Tanzania, hususan kwa mashabiki wa Yanga SC na Taifa Stars, ambako aliwahi kutumika kwenye tasnia yake ya soka.

Golikipa huyo alikuwa mahiri chini ya milingoti mitatu na alitambulika kwa nidhamu, ujasiri na uwezo mkubwa wa kuongoza safu ya ulinzi, hali iliyomfanya kuwa miongoni mwa makipa bora katika kizazi chake.

Uongozi wa Yanga SC, wanachama, wachezaji, benchi la ufundi pamoja na mashabiki na wadau wa soka wametuma salamu za pole kwa familia, ndugu na jamaa wa marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

Bwana alitoa, na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe.

Pumzika kwa amani, Peter Manyika

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments