SINGIDA BLACK STARS WAFANYA MABADILIKO, GAMONDI HURU KUHUDUMU STARS

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Uongozi wa Klabu ya Singida Black Stars umetangaza rasmi kumteua David Ouma kuwa Kocha Mkuu mpya wa klabu hiyo, akichukua nafasi ya Miguel Angel Gamondi aliyebadilishiwa majukumu na kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo, Januari 05, 2025, uteuzi wa Ouma unalenga kuimarisha benchi la ufundi na kuipa timu mwelekeo mpya katika mashindano yanayoendelea. Ouma ambaye awali alikuwa kocha msaidizi, atashirikiana na makocha wasaidizi Mousa Nd’aw na Muhibu Kanu katika jukumu la kuinoa timu hiyo.

Katika mabadiliko mengine ya kiufundi, Singida Black Stars imemwajiri Othmen Najjar kuwa Meneja Mkuu wa timu, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Ramadhani Nsanzurwimo ambaye sasa amebadilishiwa majukumu na kuteuliwa kuwa Mshauri wa Ufundi wa klabu hiyo.

Hata hivyo, uongozi wa klabu umeweka wazi kuwa haina pingamizi kuhusu Miguel Gamondi kuteuliwa kukinoa kikosi Cha Stars kama kocha wa kudumu.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments