SIMBA SC YAMTAMBULISHA KIUNGO MSHAMBULIAJI INNO LOEMBA

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Simba SC imemtambulisha rasmi kiungo mshambuliaji Inno Jospin Loemba (22), raia wa Congo Brazzaville, akitokea klabu ya Colombe Sportive ya Cameroon.

Loemba anajiunga na wekundu wa Msimbazi katika jitihada za kuimarisha kikosi hicho baada ya myumbo wa hivi karibuni huku akitarajiwa kuongeza ubunifu, kasi na nguvu mpya katika eneo la kati kwenda mbele.

Kiungo huyo chipukizi amekuwa akionesha kiwango kizuri katika soka la Cameroon, hali iliyomvutia Simba SC kumsajili mapema ili kuimarisha kikosi kwa mashindano ya ndani na ya kimataifa.

Usajili wa Loemba unaongeza ushindani kikosini na unaashiria dhamira ya Simba SC kupigania mafanikio makubwa msimu huu kilicho Baki ni mchezaji kuonyesha alichonacho uwanjani.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments