Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Simba SC inaendelea kuwapa wapinzani utamu barani Afrika baada ya kupoteza tena kwa bao 1-0 dhidi ya Esperance de Tunis wakiwa ugenini katika mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kipigo hicho kimeiweka Simba kwenye rekodi isiyofurahisha, ikiwa ndiyo timu pekee kati ya 16 zilizopo hatua hiyo iliyopoteza michezo yote bila alama hata moja , yaani ukiwekwa msimamo wa timu zinazoshiriki makundi klabu bingwa Simba itaburuza mkia.
Kwa taswira ya “kugawa utamu”, Simba kwa sasa inaonekana kugawa alama kwa wapinzani wake, hali inayowafanya wanogewe huku Wekundu wa Msimbazi wakizidi kuyumba. Matokeo hayo yameongeza presha kwa benchi la ufundi na uongozi, hasa ikizingatiwa kuwa katika michezo mitano ya mwisho, Simba imeshinda mchezo mmoja, imetoa sare moja na kupoteza michezo mitatu Hali inayoleta wasiwasi mkubwa kuhusu mustakabali wa klabu.
Kihistoria, Simba haijawahi kufikia idadi hii ya michezo ya hatua ya makundi bila alama yoyote kwenye michuano ya kimataifa, Hali hii inaashiria changamoto pana zaidi ya matokeo ya ufanisi wa safu ya ushambuliaji, uimara wa ulinzi, mipango ya kiufundi, pamoja na utayari wa kisaikolojia wa wachezaji.
Kwa mazingira haya, kikao cha dharura kinaonekana kuwa cha lazima zaidi , Uongozi unapaswa kukaa chini na kufanya tathmini ya kina kuanzia maandalizi, mbinu, uteuzi wa kikosi hadi mikakati ya mchezo kabla mambo hayajaharibika zaidi.
Mashabiki wanahitaji majibu, na klabu inahitaji mwelekeo mpya ili kurejesha hadhi yake barani Afrika na ndani ya nchi kama viongozi watazembea kuchukua hatua ya dharura klabu itapoteza hadhi yake, na hatari ya mashabiki kuisusia klabu inaonekana dhahiri, hivyo jitihata zinatakiwa kuchukuliwa mapema ikiwemo MABADILIKO ndani ya klabu kama wavyodai mashabiki.
Ikiwa Simba itaendelea “kutoa utamu” bila marekebisho ya haraka, safari ya CAF inaweza kugeuka somo litakalo waacha na uchungu, Sasa ni wakati wa kujirekebisha, kujitathimini na kuchukua hatua kabla ya kugeuzwa mchekea na Kila timu.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com




Post a Comment