SENEGAL BINGWA AFCON2025, MANE ANUSURU TASWIRA SOKA LA AFRIKA

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Senegal wameandika historia mpya ya soka la Afrika baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kufuatia ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Morocco katika fainali kali iliyojaa drama na sintofahamu za hapa na pale.

Mchezo huo uliokwenda mpaka dakika 120 za nyongeza ulihitaji uvumilivu mkubwa, nidhamu ya hali ya juu na mioyo ya chuma ili kukamilisha dakika za fainali hiyo, bao pekee la ushindi lilifungwa na Pape Gueye dakika ya 94, wakati wa dakika 120 za nyongeza.

Fainali hiyo iliingia sintofahamu Dakika ya 90+8 kipindi Cha pili baada ya Morocco kupatiwa penati tata baada ya marejeo ya VAR, uamuzi uliopingwa vikali na wachezaji wa Senegal na hii ilikuwa mara baada ya bao lao kukatakiwa muda mchache na refa hakujihusisha na kuangalia VAR lakini tukio la Brahim Diaz kuchezewa madhambi kupitia shambulio la kona haraka refa alienda chumba Cha VAR na kuamuru mikwaju wa penati Kitendo ambacho kiliwachukiza wachezaji , mashabiki na benchi la ufundi la Senegal na kuamua kususa na kutoka nje ya uwanja na kuelekea vyumba vya kubadilishia nguo.

BUSARA ZA SADIO MANE ZIKA UNUSURU MCHEZO

Baada ya sintofahamu hiyo wachezaji kwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakiomgozwa na kocha wao, lakini ikawa tofauti kwa Mane ambae alisimama imara na kuwataka wachezaji wenzake kutoka ndani ya vyumba na kurudi uwanjani , sura ya Mane ilikua ni ya ukali iliyojaa uongozi ndani yake ambapo wachezaji pamoja na benchi la ufundi walitii sauti hiyo na kurejea kukubali pigo la penati ambapo Morocco walikosa mkwaju huo na kuupeleka mpira dakika 120 ambapo ndipo Senegal walioupata ushindi wao.

Msimamo wa Mane umenusuru taswira ya soka la Afrika na inatakiwa ashukuriwe kwa busara zake, na CAF wajifunze kwenye usawa na haki ili kuondoa vitendo vya sintofahamu kwenye soka.


TUZO ZA AFCON2025

Mchezaji Bora ni Sadio Mane kutokea Senegal

Mfungaji Bora wa AFCON aliibuka kuwa Brahim Díaz, aliyefunga mabao matano (5) kutokea Morocco.

Kipa Bora wa Mashindani ni Yassine Bounou (Bono) kutokea Morocco .

Mashindano haya yatafanyika Tena 2027 kwa ushirikiano wa nchi tatu Kenya , Uganda na Tanzania.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com




0/Post a Comment/Comments