RONALDO NA SAFARI YA MABAO 1000

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Cristiano Ronaldo ameendelea kuandika historia baada ya kufunga bao moja jana usiku katika ushindi wa mabao 3-0 wa klabu ya Al Nassr wakiwa ugenini dhidi ya Al Khoolod.

Nyota huyo raia wa Ureno alitikisa nyavu dakika ya 47, bao lililo onyesha dhahiri dhamira ya nyota huyo kufunga mabao zaidi na kufikisha mabao 1000 kwenye maisha yake ya soka kama ilivyo shauku yake.

Kwa bao hilo, Ronaldo sasa amefikisha jumla ya mabao 961 katika michezo 1,308 ya maisha yake ya soka la ushindani, akiendelea kusogea karibu na rekodi ya kihistoria ya kufunga mabao 1,000 safari inayozidi kuwa halisi kila anapo zikanyaga nyasi.

Mashabiki wa Al Nassr na wapenda soka duniani wanaendelea kushuhudia hadithi ya kipekee ya mchezaji ambaye bado ana njaa ya mafanikio licha ya umri na rekodi lukuki alizovunja.


0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com


0/Post a Comment/Comments