PDD TISHIO JIPYA NBC PREMIER LEAGUE

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Utatu wa PDD (Pacome, Dube na Depu) umeibuka rasmi kwa mara ya kwanza kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa na mara moja kuacha alama nzito katika NBC Premier League, baada ya kuonyesha uwezo mkubwa ulioanza kuwatia hofu wapinzani wa Yanga SC.

Katika ushindi wa kishindo wa mabao 6-0 dhidi ya Mashujaa FC, PDD ilionekana kama silaha mpya iliyoumgana huku wachezaji hao wakitumika kama nguvu kazi kwenye safi ya ushambuliaji , Licha ya kuibuka kwa mara ya kwanza, walihusika moja kwa moja katika mabao matatu, ishara tosha kuwa muunganiko huo una uwezo mkubwa.

Kilichozidi kuvutia ni uwepo wa Depu, mchezaji mpya kikosini, ambaye licha ya kuwa bado anaanza safari yake ndani ya Yanga, ameonyesha kuendana haraka na kasi ya ligi pamoja na falsafa ya timu. Ujio wake utaongeza nguvu mpya, kasi na presha kwa safu za ulinzi za wapinzani.

Pacome na Dube, waliokwishajizolea uzoefu ndani ya ligi, walionekana kumsaidia Depu kuingia kwenye mfumo kwa haraka, na kufanya PDD ionekane kama utatu uliokaa pamoja kwa muda mrefu, jambo lililowashangaza wengi.

Kwa kuibuka kwake kwa mara ya kwanza na kuonyesha mafanikio haraka, PDD sasa imekuwa tishio jipya kwa wapinzani wa Yanga sio kwa maneno tu hata wapinzani wakubwa wa Yanga , klabu ya Simba Kwa upande wa mashabiki zake wamekiri kuwa wananchi wameimarika huku wao wakibaki kulia na uongozi wao.

Kwa mwenendo huu, PDD inaashiria mwanzo mpya ya ushindani ndani ya kikosi cha Yanga, huku wapinzani wakianza kutafakari kwa kina namna ya kukabiliana na Wananchi ambao sasa wana silaha mpya ambazo ni hatari kwa wapinzani.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments