OKELLO BALAA JIPYA JANGWANI

 


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Young Africans SC imefanikiwa kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji, Allan Okello (25) mchezaji wa kimataifa kutoka Uganda, hatua inayotajwa kuongeza ubunifu, kasi na ubora katika safu ya kiungo ya Wananchi.

Okello, anatua Yanga akitokea Vipers SC ya Uganda, ni miongoni mwa viungo wanaoheshimika zaidi Afrika Mashariki kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuchezesha timu, kupiga pasi za mwisho na kufunga mabao, Mbali na mafanikio yake ngazi ya klabu, Okello pia ni nguzo muhimu kwa Timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes), ambako ameendelea kuonyesha kiwango cha juu katika mashindano ya kimataifa.

Kwa mtazamo wa kiufundi, Okello ni mchezeshaji, mchezaji mwenye akili ya hali ya juu ya mpira, ana uwezo wa kusoma mchezo, kutuliza tempo, kugawa mipira kwa usahihi na kuleta hatari kubwa katika robo tatu ya mwisho ya uwanja Uwezo wake wa kupiga mashuti makali akiwa nje na ndani ya boksi, pamoja na mipira ya adhabu, unampa hadhi ya kiungo namba 10 wa kisasa.

Tofauti na viungo wengi wa kawaida, Okello anaweza kucheza katika nafasi zaidi ya moja ana uwezo wa kucheza katikati, pembeni (winga ya kulia au kushoto) jambo linaipa Yanga chaguo pana la kiufundi Uwezo wake wa kubadilika, kasi na ufundi unatarajiwa kuipa Yanga silaha mpya katika mashindano ya ndani na kimataifa.

Ujio wa Okello Jangwani unatazamwa kama kiungo muhimu katika mpango wa Yanga kuendelea kutawala soka la Tanzania na kufanya vizuri zaidi kwenye michuano ya Afrika.

Mashabiki wa Wananchi sasa wanatarajia kuona ushirikiano wake na nyota wengine wa timu, huku matumaini yakiongezeka kuwa ubunifu wa safu ya mbele utaimarika kwa kiwango kikubwa.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments