Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Mtibwa Sugar imeondoka na alama moja muhimu baada ya kuilazimisha Simba SC sare ya mabao 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochezwa kwenye Dimba la Meja Jenerali Isamuhyo.
Matokeo hayo yamekuwa pigo jingine kwa wekundu wa Msimbazi, ambao wameendelea kuyumba baada ya kudondosha alama kwa mchezo wa pili mfululizo katika mbio zao za kuwania ubingwa wa ligi msimu huu baada ya kufungwa 2-0 na Azam fc Leo wamelazimishwa Sare ikiwa wanapoteza alama nne kwenye michezo miwili huku Sare hiyo ikizidi kuongeza presha kwa Simba, hasa ikizingatiwa kuwa walikuwa wakicheza nyumbani mbele ya mashabiki wao.
Simba waliingia uwanjani kwa dhamira ya kupata ushindi, wakitawala umiliki wa mpira na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga. Juhudi zao zilizaa matunda walipopata bao la kwanza kipindi cha kwanza 20' kupitia kwa Elie Mpanzu lililowapa matumaini ya kuondoka na pointi zote tatu.
Hata hivyo, Mtibwa Sugar walionyesha ujasiri na nidhamu kubwa kipindi cha pili huku walibadili mbinu, wakiongeza mashambulizi na kutumia vyema nafasi waliyoipata dakika ya 61 kupitia kwa Fredrick Magata kuweka mzani sawa na kuwanyamazisha wapinzani wao
Sare hiyo imeifanya Simba kuendelea kudondosha alama muhimu katika Ligi Kuu ya NBC, hali inayoweza kuwaathiri katika mbio za ubingwa, huku Mtibwa Sugar wakionja utamu wa kuvuna alama dhidi ya Simba kwa kupata sare wakiwa ugenini.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment