MCHEZA KWAO HUTUNZWA, MBELEKO YATUMIKA KUIPELEKA MOROCCO ROBO FAINALI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Timu ya Taifa ya Morocco imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania katika mchezo wa hatua ya 16 Bora.

Morocco, ambaye ni mwenyeji wa mashindano hayo, ilipata bao lake pekee katika kipindi cha pili cha mchezo kupitia Brahim Diaz 64' bao lililodumu hadi filimbi ya mwisho na kuwafanya Simba wa Atlas kuendelea na safari yao ya AFCON 2025.

Hata hivyo, ushindi huo umeacha mjadala mkubwa kuhusu maamuzi ya referee wa mchezo huo Boubou Traore baada ya dakika ya 90+3, Tanzania kunyimwa penalti iliyodaiwa kuwa ya wazi baada ya Iddy Nado kuangushwa ndani ya eneo la hatari.

Kilichozua mshangao na hasira kwa benchi la ufundi pamoja na mashabiki wa Tanzania ni referee kushindwa kutumia teknolojia ya VAR kuangalia tukio hilo muhimu, licha ya umuhimu wake katika dakika za nyongeza lakini refa huyo hakutaka kujihusisha kuangalia tukio Hilo ambalo linge warejesha stars mchezoni lakini haikuwa hivyo.

Licha ya presha kubwa iliyowekwa na Tanzania katika dakika za mwisho, haikufanikiwa kupata bao la kusawazisha, na hivyo kuhitimisha safari yao ya AFCON 2025 katika hatua ya 16 Bora.

Traore na historia ya ushindi dhidi ya Morocco

Refa huyu amechezesha michezo nane iliyo ihususha Morocco na katika michezo hiyo yote ilimalizika kwa timu hiyo kupata ushindi ikiwemo hapo Jana, na ametoa penati tatu ambazo zote ziliwapa faida Morocco.

Kwa matokeo hayo, Morocco inaendelea na mashindano, huku Tanzania ikiondoka kishujaa ikiwa imefanya vizuri kwa mara ya kwanza toka AFCON imeanza lakini ikiwa na maswali mengi juu ya maamuzi ya referee yaliyoathiri matokeo ya mchezo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com




0/Post a Comment/Comments