MASHINDANO YA CHAN YAFUTWA

 


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limetangaza rasmi kusitisha kuchezwa kwa Michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), uamuzi uliokuja baada ya tathmini ya kina ya kalenda ya soka na changamoto za upangaji wa mashindano hayo.

Uamuzi huo ulitangazwa na Rais wa CAF, Dkt. Patrice Motsepe, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika nchini Morocco, Ijumaa Januari 17, Akizungumza katika mkutano huo, Dkt. Motsepe alieleza kuwa sababu kuu ya kusitishwa kwa CHAN ni msongamano mkubwa wa ratiba ya mashindano ya soka barani Afrika na kimataifa pamoja mashindano kuingiza hasara.

Rais huyo wa CAF alifafanua kuwa katika kipindi kijacho, kutakuwa na mabadiliko makubwa kwenye kalenda ya soka ya bara la Afrika, ambapo mashindano mapya na marekebisho ya ratiba yatafanyika ili kutoa nafasi kwa michuano yenye ushindani na mvuto zaidi.


Aidha, Dkt. Motsepe alisisitiza kuwa CAF inalenga kuimarisha uhusiano wake na mashirikisho ya soka ya kimataifa, kwa kuhakikisha kunakuwepo uhuru, uwazi na ushirikiano wa kweli badala ya migawanyiko, jambo litakalosaidia kukuza maendeleo ya soka la Afrika kwa ujumla.

Uamuzi wa kusitishwa kwa CHAN umeibua mjadala mpana miongoni mwa wadau wa soka, hasa kwa nchi ambazo zimekuwa zikitegemea michuano hiyo kama jukwaa la kukuza na kuonyesha vipaji vya wachezaji wa ligi za ndani. 

Hata hivyo, CAF imeahidi kuja na mbinu mbadala zitakazohakikisha vipaji hivyo vinaendelea kuendelezwa na kupewa fursa stahiki katika majukwaa ya kimataifa.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments