MAN CITY YAMTAMBULISHA ANTOINE SEMENYO

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Manchester City imekamilisha usajili wa winga wa kimataifa wa Ghana, Antoine Semenyo, kutoka klabu ya AFC Bournemouth kwa ada ya pauni milioni 62.5 sawa na euro milioni 72.

Semenyo mwenye (26 ) amesaini  mkataba wa kuitumikia Man City hadi Juni 2031, ambapo atavaa jezi namba 42, Nyota huyo anatarajiwa kuongeza ushindani na nguvu katika safu ya ushambuliaji ya mabingwa hao wa England kutokana na kasi, nguvu na uwezo wake wa kufumania nyavu.

Kwa mujibu wa makubaliano ya uhamisho huo, Bournemouth itanufaika kwa kupata asilimia 10 ya mauzo ya baadaye ya mchezaji huyo endapo atauzwa tena, pia klabu ya Bristol City, ambayo ni klabu ya zamani inatarajiwa kupokea pauni milioni 1.5 kama sehemu ya kipengele cha mauzo ya baadaye.

Usajili wa Semenyo unaonyesha dhamira ya Man City kuendelea kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao wa mashindano huku mashabiki wakisubiri kuona mchango wake ndani ya uwanja.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.

0/Post a Comment/Comments