JANUARI 18 KUMPATA SHUJAA MPYA WA SOKA LA AFRIKA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mashindano ya AFCON2025 yanakwenda kufikia kilele chake Januari 18, 2026 , pale bingwa mpya atakapopatikana kati ya wenyeji Morocco na mabingwa watetezi Senegal, baada ya timu hizo mbili kufuzu katika michezo ya nusu fainali.

Senegal walitinga fainali baada ya kuifunga Misri 1-0, bao pekee likifungwa na nyota wao Sadio Mane kwa shuti kali lililokatiza matumaini ya Mafarao , mchezo huo ulikuwa wa ushindani mkubwa, lakini uzoefu na ubora wa Senegal uliwapa tiketi ya kucheza fainali.

Kwa upande mwingine, Morocco walionyesha uimara wa hali ya juu mbele ya Nigeria katika pambano lililodumu kwa dakika 120 bila mshindi baada ya sare tasa, hatimaye, Simba wa Atlas wakailinda heshima ya uwenyeji wao kupitia mikwaju ya penati 4-2, na kuamsha furaha kwa mashabiki wao walio jaa Kila kina ya uwanja.

Kwa ratiba, mchezo wa mshindi wa tatu utafanyika Januari 17, ambapo Misri watavaana na Nigeria kupigania heshima ya nafasi ya tatu huku Siku moja baadaye, Januari 18, macho na masikio ya Afrika nzima yataelekezwa kwenye fainali kati ya wenyeji Morocco dhidi ya Senegal mchezo unaotarajiwa kuwa wa kasi, na mbinu zaidi.

Je, Morocco wataandika historia nyumbani kwa kunyakua taji mbele ya mashabiki wao? Au Senegal wataendelea kutawala na kuthibitisha ubabe wao barani Afrika Januari 18 itatoa jibu huku Afrika itapata shujaa mpya wa soka.


0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments