Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Hatua ya nusu fainali ya AFCON 2026 si tu kuhusu majina makubwa, bali ni mgongano wa falsafa za soka, mifumo ya uchezaji na ubora wa mtu mmoja mmoja. Morocco vs Nigeria na Egypt vs Senegal ni mechi mbili zinazobeba uzito wa fainali kabla ya fainali.
Hatua hii inatarajiwa kufanyika Januari 13 , 2025 ambapo wababe wawili wanatarajiwa kutinga hatua ya fainali kwaajili ya kumtafita bingwa.
MOROCCO vs NIGERIA
Morocco
Morocco wanaingia mechi hii wakiwa na mpangilio uliokomaa. Wanacheza soka la kumiliki mpira, kujenga mashambulizi kwa utulivu na kutumia vyema maeneo ya pembeni wakiomgozwa na Achraf Hakimi ni mchezaji wa ziada wa kiungo anayevunja ulinzi wa wapinzani kwa mbio na pasi za mwisho, Morocco hutengeneza idadi kubwa ya nafasi kupitia kupanda kwa mabeki wa pembeni na kuingia kwa viungo washambuliaji.
Changamoto yao kubwa ni kulinda nafasi wanazoacha nyuma ya mabeki wao wa pembeni Kila wanapo panda nyuma kunabaki pengo linaloweza kutumiwa na Nigeria kutengeneza hatari ya bao.
Nigeria
Nigeria hawahitaji kumiliki mpira kwa muda mrefu. Wanahitaji nafasi chache tu mchezaji kama Victor Osimhen ni straika anayechanganya nguvu, harakati na umaliziaji wa kiwango , Nigeria wanatafuta mpira wa haraka kwenda mbele, wakiwapa washambuliaji nafasi ya kukimbia nyuma ya mabeki.
Udhaifu wa Nigeria uko kwenye ulinzi wa pembeni wanapokabili timu inayocheza kwa upana kama Morocco.
.
EGYPT vs SENEGAL
Egypt
Egypt ni timu inayojua kushinda mechi kubwa bila kuonekana bora muda wote Wanacheza kwa tahadhari, wakilinda safu ya nyuma kwa nidhamu na kusubiri makosa ya mpinzani wakitegemea mipira ya kutenga na mashambulizi ya kushitukiza kupitia Salah na Marmush washambuliaji wenye Kasi wakiwa na mpira.
Tatizo la Egypt ni kutegemea zaidi washambuliaji wao wa pembeni ili kuwapatia matokeo kama wapinzani wao wakishikilia vizuri washambuliaji wa pembeni Egypt watakuwa na wakati mgumu kwenye kupata matokeo.
Senegal
Senegal wanacheza soka la nguvu, kasi na presha ya juu Safu yao ya kiungo ni imara, inakata mipira mapema na kuanzisha mashambulizi ya haraka huku wakimiliki mpira na kufanya mashambulizi muda mwingi wa mchezo.
Udhaifu wao unaweza kuwa kujisahau kwa kushambulia, wakiacha nafasi ambazo washambuliaji wa Egypt wanaweza kuzitumia kama udhaifu na kundikisha bao.
Mwelekeo wa Mchezo
Egypt watacheza kwa kujilinda wakisubiri mipira ya adhabu na mashambulizi ya kushitukiza
Senegal watashambulia kwa idadi kubwa ya wachezaji.
Mchezaji mmoja anaweza kubadili historia: Osimhen, Hakimi, Salah au Mane
Atakayekuwa makini zaidi na kutumia nafasi atakazo zipata atatinga fainali ya AFCON 2026.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.





Post a Comment