Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Ligi Kuu ya England (EPL) bado iko wazi na mbio za ubingwa zimechukua sura mpya baada ya Arsenal, kinara wa ligi, kupoteza kwa mabao 3-2 dhidi ya Manchester United kwenye Uwanja wa Emirates kwenye mzunguko wa 23 wa ligi hiyo.
Matokeo hayo yamepunguza pengo la alama kati ya Arsenal na wawaniaji wake wakuu ambao ni Manchester City na Aston Villa hadi alama nne , tofauti inayoweza kufikiwa kwa wastani wa michezo miwili endapo vinara watadondosha alama na wapinzani kufanya vizuri.
Kipigo hicho kimeitikisa Emirates na kuamsha upya matumaini ya City na Villa, timu ambazo nazo bado hazijawa na mfululizo mzuri wa matokeo lakini kupoteza kwa Arsenal kunawafanya wasogee kukielekea kikombe.
City, ni timu yenye uzoefu wa kukimbiza ubingwa na mara kadhaa wamekuwa wakishinda mbio hizo dakika za mwisho jambo ambalo linatakiwa kuchukuliwa kama tahadhari na Arsenal, huku Villa nao wakijitutumua kundikisha historia msimu huu.
Kwa upande mwingine, ushindi huo umeipa Manchester United tiketi ya kuingia nne bora baada ya mapambano ya muda mrefu msimu huu, United wameonyesha tabia ya kupambana hadi mwisho, na ushindi dhidi ya Arsenal umeongeza kujiamini na kuimarisha nafasi yao katika mbio za juu ya jedwali tumaini lao likiwa ni kuhakikisha wanaocheza UEFA champions league msimu ujao.
Kwa Sasa macho yote yanaelekezwa kwa Arsenal huku swali likiwa ni je, watahimili presha na kulinda kilele hadi mwisho, au historia itajirudia wakifanya kawaida yao ya kuukosa ubingwa dakika za jioni? Majibu yatategemea uimara wa kikosi, maamuzi ya benchi la ufundi, na uwezo wa kukusanya alama muhimu kwenye michezo iliyosalia.
Kwa sasa, EPL bado mbichi na ubingwa haujapata mwenyewe Mbio zinaendelea, presha inaongezeka, na mashabiki wanasubiri kwa hamu kuona nani atatwaa taji la EPL.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com



Post a Comment