DORGU NJE KWA WIKI 10

 


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Manchester United imethibitisha kuwa beki wake wa pembeni Patrick Dorgu, atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki 10 kutokana na jeraha la nyama za paja (hamstring).

Dorgu alipata jeraha hilo kwenye mchezo dhidi ya Arsenal, ambapo United iliibuka na ushindi wa mabao 3-2., Licha ya kuumia, mchezaji huyo alionyesha moyo wa kishujaa baada ya kufunga bao la pili lililochangia ushindi huo muhimu kwa klabu yake.

Vipimo vilivyofanywa baada ya mchezo vimebaini jeraha hilo ni kubwa, hali itakayomuweka nje kwa takribani miezi miwili na nusu Kukosekana kwake ni pigo kwa Manchester United, hasa ikizingatiwa alikuwa katika kiwango bora kipindi ambacho united ilikua inarejea kwenye ubora wake.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments