BARCELONA WATWAA UBINGWA MBELE YA MADRID

 

Timothy Lugembe ,

Mwanakwetusports .

Barcelona wameandika historia nyingine mbele ya mahasimu wao wa jadi Real Madrid baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 na kutwaa taji la SuperCopa de Espana 2026, katika fainali ya kusisimua iliyopambwa na hisia kali za El Clásico iliyopigwa nchini Saud Arabia.

Mchezo huo ulianza kwa tahadhari kutoka pande zote mbili, lakini Barcelona wakawa wa kwanza kuufungua ukurasa wa mabao dakika ya 36 kupitia Raphinha, aliyefunga kwa ustadi na kuamsha shangwe kwa mashabiki wa Barcelona, Real Madrid hawakusubiri , Vinicius Jr akasawazisha dakika ya 45+1 na kufanya mchezo uwe kwenye mzani sawa.

Hata hivyo, kabla moshi wa bao la kusawazisha haujatulia, Barcelona waliongeza bao la pili kupitia Robert Lewandowski aliyefunga dakika ya 45+3, bao lililowapa uongozi wa 2-1, Madrid walipata bao la pili dakika za nyongeza (45+5), na kurejea mchezoni.

Kipindi cha pili kilishuhudia Madrid wakiongeza kasi wakisaka bao la kusawazisha, lakini Barcelona walikuwa makini na hatari zaidi mnamo dakiika ya 73, Raphinha aliibuka tena na kufunga bao lake la pili, akiweka muhuri wa mchango wake mkubwa na kuifanya Barca waongoze 3-2 matokeo yaliyodumu kwa dakika zote tisini.

Kwa ushindi huo, Barcelona wametwaa SuperCopa de España 2026, wakithibitisha ubora wao mbele ya Real Madrid na kumpa Raphinha nafasi ya kukumbukwa kama shujaa wa usiku wa dhahabu Ushindi huu unaipa Barca mwanzo mzuri wa mafanikio katika msimu unaoendelea.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments