Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Wachezaji wa klabu ya Simba SC, Jonathan Sowah na Allasane Kante, wamefungiwa kucheza michezo mitano kila mmoja pamoja na kutozwa faini ya Sh milioni moja, kufuatia vitendo visivyo vya kiuanamichezo vilivyojitokeza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Azam FC.
Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), baada ya Sowah kupatikana na kosa la kumpiga kiwiko kiungo wa Azam FC, Himid Mao Mkami , Kwa upande wake, Kante ameadhibiwa kwa kosa la kumpiga teke kwa makusudi kiungo wa Azam FC, Feisal Salum "Fei toto".
Vitendo hivyo vilitokea katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, ambapo Simba SC walikubali kichapo Cha 2-0.
Katika uamuzi mwingine, TPLB imemfungia kiungo wa Singida Black Stars, Khalid Aucho, michezo mitano na kumtoza faini ya Sh milioni moja kwa kosa la kumpiga na kumsukuma mchezaji wa TRA United, Adam Adam, wakati wa mchezo uliomalizika kwa Singida Black Stars kupata ushindi wa 3-1.
Maamuzi hayo yamekuja ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha nidhamu na kulinda maadili ya mchezo wa soka katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment