Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Michuano ya UEFA champions league inaendelea kushika Kasi katika mzunguko wa sita ambapo maji na mafuta tayali yameanza kujitenga kuelekea hatua ya 16 Bora.
Wiki hii imepigwa michezo ambapo imeshuhudiwa vilabu Vikianguka vingine kuinuka kwenye mfululizo wa matokeo.
Inter Milani 0-1 Liverpool
Mchezo ulipigwa katika dimba la San Siro ikishudiwa majogoo wakiamka usingizinu mwa matokeo mabovu na kuchukua alama zote mbele ya wanafainali msimu ulio pita, ushindi unao waweka nafasi ya tisa alama 12, huku Inter wakiwa nafasi ya 6 alama 12 tofauti ikiwa magoli ya kufunga na kufungwa.
Real Madrid 1-2 Man city
Klabu ya Real Madrid imepoteza mchezo wa pili mfululizo ambapo kwenye michezo mitano imepoteza miwili , sare Moja na ushindi mara mbili huku Pep akizidi kuendeleza ufalme wake pale Bernabeu akiwa ni kocha ambae ameifunga Madrid mara nyingi zaidi Bernabeu ikiwa ni mara ya Saba.
ARSENAL YAZIDI KUJIKITA KILELENI BILA KUFUNGWA
Klabu ya Arsenal imezidi kuonyesha dhamira Yao ya kuwania kikombe ikiwa ni timu pekee mpaka sasa iliyoshinda michezo yote ambapo hapo Jana waliibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya club Bruge matokeo yanayo waweka kileleni mwa msimamo.
0767815473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment