TRENT NJE KWA MAJERAHA , CAMAVINGA HALI SIO MBAYA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Real Madrid imepata pigo baada ya taarifa kuwa msimu wa 2025 wa beki wao, Trent Alexander Arnold, huenda ukawa umekwisha kufuatia jeraha la enka ambalo linaelezwa kuwa kubwa na la kutia wasiwasi.

Kwa mujibu wa kituo cha taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika Trent anatarajiwa kupumzishwa kwa wiki kadhaa huku uchunguzi wa mwisho ukitarajiwa kufanyika leo.

Kwa upande mwingine, ndani ya Madrid kuna hali ya utulivu kuhusu kiungo Eduardo Camavinga, ambapo taarifa kutoka benchi la ufundi zinaeleza kuwa jeraha lake halionekani kuwa zito kiasi cha kumuweka nje kwa muda mrefu.

Real Madrid inatarajia kumrejesha uwanjani hivi karibuni endapo ataendelea vizuri katika hatua za matibabu.

0767915474,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments