Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Real Madrid imekubali kichapo Cha 2–0 nyumbani dhidi ya Celta Vigo kwenye La Liga, mchezo uliopigwa Bernabeu ambapo Madridi walilazimika kumaliza mchezo wakiwa pungufu kufuatia kuonyesha kadi nyekundu kwa wachezaji wao wawili.
Celta walipata mabao yote kipindi cha pili kupitia Williot Swedberg 53' , 90+3 nakupeleka msiba kwa Madridi huku akiwapatia alama tatu muhimu Celta.
Madrid ilipata pigo dakika ya 24 baada ya Eder Militao kutolewa kwa jeraha la misuli na kulazimisha safu ya ulinzi kubadilishwa.
Madrid ilizidi kuyumba dakika ya 62 baada ya Fran Garcia kutolewa kwa kadi mbili za njano ndani ya dakika mbili.
Katika muda wa nyongeza, Alvaro Carreras naye alipewa kadi nyekundu kwa malalamiko kupita kiasi kwa mwamuzi, na kuwaacha Madrid wakiwa tisa uwanjani.
Kipigo hicho kimeiacha Madrid nyuma ya Barcelona kwa pointi nne, huku Celta wakipanda nafasi ya 10 wakiwa na pointi 19.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com




Post a Comment