STARS YAWEKA HISTORIA, YATINGA HATUA YA 16 BORA AFCON KWA MARA YA KWANZA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imeandika historia mpya kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kufuzu kwenda hatua ya 16 bora kwa mara ya kwanza tangu kushiriki kwake kwenye michuano hiyo.

Stars ilikata tiketi hiyo baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Tunisia katika mchezo wa mwisho wa Kundi C uliochezwa jana, matokeo yaliyoiwezesha kusonga mbele kama miongoni mwa timu bora zilizomaliza nafasi ya tatu (‘best losers’) wakiwa na alama mbili.

Katika hatua ya 16 Bora Stars watamenyana na wenyeji Morocco Januari 4, 2026 , mchezo ukitarajiwa kuwa mgumu kutokana na kuongezeka kwa ubora kiuchezaji kwa Stars huku Morocco wakijivunia faida ya nyumbani wakicheza mbele ya mashabiki zao.

Katika mchezo huo, Tunisia walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia Gharbi dakika ya 43, kabla ya Feisal Salum ‘Feitoto’ kuibuka shujaa wa Stars kwa kusawazisha bao hilo dakika ya 48, akirejesha matumaini kwa Watanzania na hatimaye kuandika historia katika soka barani Afrika.

Kwa matokeo hayo, Tanzania imeungana na Nigeria pamoja na Tunisia kufuzu hatua ya 16 bora kutoka Kundi C la AFCON 2025, hatua inayochukuliwa kama mafanikio makubwa katika historia ya soka la taifa.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com




0/Post a Comment/Comments