STARS YAPOTEA MBELE YA NIGERIA SOKA LAONEKANA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mchezo wa kwanza kundi C Afcon uliowakutanisha Taifa stars dhidi ya Nigeria umemalizika kwa stars kukubali kichapo Cha 2-1 kwenye mchezo wa kwanza wa kundi hilo.

Licha ya kupoteza mchezo huo Stars walionyesha kiwango bora kwa kutengeneza nafasi nyingi ila umakini eneo la umaliziaji uliwakosesha matokeo, katika mchezo huo Stars walikosa nafasi nne za wazi na kupelekea kupoteza mchezo huo, Kwa upande mwingine eneo la nidhamu limeimarika baada ya dakika tisini kumalizika bila kadi yeyeote.

Stars imeonyesha kiwango kizuri kuanzia eneo la umiliki wa mpira na kutengeneza mashambulizi wamekuwa Bora ukizingatia wamecheza na Moja ya timu bora yenye wachezaji wenye uzoefu mkubwa wakisoka katika ligi mbali mbali barani ulaya.

Kwenye mchezo huo kipa wa Stars Zuberi Foba alioonyesha kiwango bora licha ya kuruhusu bao mbili , na viatu vya Tanzania one vinaonekana kumtosha kulingana na uwezo wake wa kupiga pasi, kuokoa michomo na kuanzisha mashambulizi , vyote hivyo amevionyesha na kufufua matumaini ya Wengi kuwa huenda akachukuwa nafasi hiyo chini ya kocha Miguel Gamond.

Matokeo mengine ya kundi C ni

Tunisia 3-1 Uganda

Kundi D

D.R Congo 1-0 Benin

Senegal 3-0 Botswana



0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments