AAGA KWA MANENO YA UPENDO
Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Aliyekuwa nahodha na mshambuliaji wa Tottenham Heung-Min Son, ameaga rasmi klabuni hapo kwa heshima ya kipekee baada ya kutumikia klabu hiyo kwa zaidi ya muongo mmoja uliosheheni mafanikio.
Hafla maalumu ya kumuaga ilifanyika katika Uwanja wa Tottenham Hotspur na kuwavutia maelfu ya mashabiki waliompa heshima ya kipekee wakati wa mchezo wa UCL dhidi ya Slavia Prague ambapo walishinda 3-0.
Katika tukio hilo lenye hisia kali, Son aliandaa barua ya upendo kwa mashabiki wa Spurs, akitoa ujumbe mzito uliogusa mioyo ya mashabiki Wengi.
“Natumaini hamjanisahau imekuwa miaka 10 ya ajabu na isiyoaminika nilichotaka ni kusema asante nitabaki kuwa Spur daima, na daima nipo pamoja nanyi,” alisema mbele ya mashabiki wa Spurs.
Son aliendelea kusisitiza namna klabu hiyo ilivyokuwa sehemu muhimu ya maisha yake ndani na nje ya uwanja.
“Hiki kitabaki kuwa nyumbani kwangu sitaweza kuwa sahau, kamwe,” aliongeza
Kwa mashabiki wa Tottenham, kuondoka kwa Son ni mwisho wa enzi ya mchezaji aliyeipigania jezi yao kwa moyo, nidhamu na kipaji cha hali ya juu Lakini kwa maneno yake, inaonekana wazi kuwa uhusiano kati yake na Spurs utadumu milele.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment