SALAH AREJEA KIKOSINI BAADA YA SINTOFAHAMU YA HIVI KARIBUNI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mohamed Salah leo amerejea rasmi katika kikosi cha Liverpool kilichokutana na Brighton wakishinda 2-0 uwanja wa Anfield, licha ya kuanza mechi hiyo akiwa benchi, nyota huyo raia wa Misri alijumuishwa kwenye kikosi baada ya kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na kocha Arne Slot, yaliyoweka wazi msimamo wa pande zote na kuweka mambo sawa.

Uamuzi wa kumweka benchi ulilenga kumpa nafasi ya kurejea taratibu huku akijiandaa na safari ya kuelekea AFCON itakayoanza wiki ijayo, hata hivyo, uwepo wake kwenye kikosi umeonyesha kuwa Salah bado ni srhemu ya kikosi hicho licha ya taarifa zilizo muhusisha kuaga klabuni hapo.

Kocha Arne Slot amesisitiza kuwa mazungumzo yalikuwa chanya na yalilenga maslahi ya timu , Liverpool sasa inaendelea na ratiba yake ikiwa na matumaini ya kupata mchango wa Salah kuelekea kwenye michezo ijayo akiwa na majogoo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com


0/Post a Comment/Comments