PACOME, DUBE WAIZAMISHA FOUNTAIN GATE

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

 Dakika 90 za mchezo kati ya Yanga SC na Fountain Gate uliopigwa katika Uwanja wa KMC Complex umemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa 2-0 , baada ya Pacome na Prince Dube kuingia nyavuni.

Bao la kwanza lilipatikana dakika ya 30 kupitia mkwaju wa penati uliowekwa kimiani na Prince Dube, baada ya shinikizo la mashambulizi ya Yanga kuilazimisha safu ya ulinzi ya Fountain Gate kufanya makosa ndani ya eneo la hatari.

Fountain Gate walijaribu kurudi mchezoni kwa kutafuta utulivu katikati, lakini ukuta wa Yanga uliokuwa imara uliwazuia mara kwa mara, huku Yanga wakitawala umiliki na kutumia vyema mipira ya pembeni.

Kipindi cha pili kilishuhudia kasi ikiongezeka, na ndipo Pacome 81' alipofunga bao la pili katika , akimalizia shambulizi la kasi lililowavunja nguvu Fountain ambao walikuwa wakisaka angalau sare ya kuwapa matumaini.

Ushindi huo unawafanya Yanga kufikisha alama 13 michezo mitano , nyuma alama nne dhidi ya JKT Tanzania anae ongoza ligi kwa alama 17 michezo 10.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com


0/Post a Comment/Comments