NIGERIA YAFUZU , HATIMA YA STARS 16 BORA HII HAPA

 

Timothy Lugembe,

MMwanakwetusports.

Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa stars) imetoshana sare ya 1-1 dhidi ya Uganda katika mchezo wa pili Kundi C , AFCON2025, huku Nigeria wakikata tiketi kucheza hatua ya 16 bora baada ya kuibamiza Tunisia 3-2.

 Stars wamevuna alama moja baada ya michezo miwili waliyocheza huku wakibakiza mchezo mmoja dhidi ya Tunisia ambao ndio utakaomua hatima yao kufuzu hatua inayofuata.

Ili Stars ifuzu 16 bora italazimika kupata ushindi dhidi ya Tunisia kwenye mchezo wa mwisho huku dua ikiwa ni kuiombea Nigeria ipate ushindi au sare dhidi ya Uganda ,

Mchezo wa Stars dhidi ya Tunisia unatarajiwa kuwa mgumu kutokana na uhitaji wa alama kwa timu zote hiyo ni kutokana na matokeo ya mwisho waliyo yapata ambapo Tunisia walikubali kipigo cha 3-2 dhidi ya Nigeria, hivyo ushindi kwa timu yoyote utafungua njia kuelekea hatua inayofuata .

Katika Kundi C tayali Nigeria imefuzu 16 bora , na mchezo wa mwisho watamaliza dhidi ya Uganda ambao wanahitaji alama tatu ili wasonge hatua inayofuata ikitegemeana namatokeo watakayo yapata wapinzani wao.


MATOKEO MENGINE KUNDI D NI

Benin 1-0 Botswana

Senegal 1-1 D.R. Congo.

0767915473,

lugembetimothy@gmail.com


0/Post a Comment/Comments