Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Prince Dube amezidi kung'ara baada ya kupachika bao pekee na la ushindi dhidi ya Costal Union kwenye mchezo wa ligi kuu NBC katika dakika ya 88' na kufanya mchezo kumalizika kwa ushindi wa 1-0.
Ushindi huo unawafanya wananchi kukisogelea kilele Cha ligi baada ya kujikusanyia alama 16 katika michezo sita wakipanda mpaka nafasi ya pili alama moya dhidi ya JKT Tanzania wanaongoza ligi hiyo.
Baada ya mfululizo wa kushindwa kukwamisha mpira kimiani Dube, alipokea lawama nyingi kutoka kwa mashabiki kitu ambacho kwa mchezaji kinashusha morali , lakini ameibuka na kuwabeba wananchi katika michezo migumu na kuwapa alama tatu.
Mchezo wa klabu bingwa dhidi ya Far Rabat alifunga bao la pekee na la ushindi na kupeleka alama tatu muhimu Jangwani, mchezo dhidi ya Fountain gate kwenye ushindi wa 2-0, alipachika bao la kwanza na Jana dhidi ya Costal Union wakati mambo yanaelekea kua ndivyo sivyo kwa wananchi mwanamfalme aliinuka na kunusuru jahazi kwa kufunga bao la pekee na la ushindi.
Baada ya kelele za muda sasa mwana Mfalme Prince Dube amerudi na anaifanya kazi yake Jangwani.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment