MWALIMU ACHUKUA NAFASI YA SOPU AFCON 2025

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mshambuliaji wa klabu ya Wydad aliyepo Simba Sc kwa mkopo, Selemani Mwalimu ‘Gomez’, ameitwa kujiunga na kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars) kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 nchini Morocco.

Kocha wa Stars, Miguel Angel Gamondi, amemjumuisha Gomez kwenye orodha ya wachezaji 28 watakaotetea heshima ya Tanzania, akichukua nafasi ya mshambuliaji Abdul Suleiman 'Sopu' aliewekwa nje kutokana na majeraha aliyoyapata Wakati wa maandalizi kuelekea mashindano hayo.

Uwepo wa Gomez unatarajiwa kuongeza nguvu kwenye kikosi Cha Stars huku uzoefu wake mkubwa alioupata kwenye mashindano ya vilabu ulimwenguni ukitarajiwa kuwa chachu kuongeza kitu kwenye kikosi.

Taifa Stars inaendelea na kambi ya maandalizi kabla ya kuelekea kwenye michuano hiyo mikubwa, huku mashabiki wakitarajia kuona mabadiliko chanya ndani ya kikosi.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments