MSUVA AIFIKIA REKODI YA MRISHO NGASSA

 

Timothy Lugemba,

Mwanakwetusports.

Mshambuliaji wa Tanzania (Taifa Stars) Simon Msuva (32) amefikia rekodi ya Mrisho Ngassa katika upachikaji wa mabao timu ya taifa kwa muda wote.

Msuva ameifikia rekodi hiyo mara baada aya kufunga bao kwenye sare ya 1-1 dhidi ya Uganda na kufikisha jumla ya mabao 25 idadi sawa na Ngassa, Msuva anahitaji bao moja ili kuivunja rekodi hiyo na kuwa mfungaji bora wa muda wote kaatika timu ya taifa.

Ubora wa mchezaji huyo katika kupachika mabao hautii shaka kwani katika AFCON tatu alizoshiriki zote amefanikiwa kupachika bao .

AFCON 2019 dhidi ya kenya

AFCON 2023 dhidi ya Zambia

AFCON 2025 dhidi ya Uganda

0767915473,

lugembetimothy@gmail.com




0/Post a Comment/Comments