Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Timu ya Taifa ya Msumbiji The Mambas imeandika historia katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada ya kuibuka na ushindi wa kwanza kufuatia ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Gabon katika mchezo wa Kundi F .
Katika mchezo huo, Gabon ilipata mabao kupitia kwa Pierre-Emerick Aubameyang aliyefunga dakika ya 45+5 na Moussounda dakika ya 76.
Mabao ya Msumbiji yalifungwa na Bangal dakika ya 37, Catamo aliyefunga kwa mkwaju wa penalti dakika ya 42 na Diogo Calila aliyefunga bao la ushindi dakika ya 52, na hivyo kuwapa The Mambas ushindi wa kihistoria toka kuanzishwa kwa mashindano hayo.
Wakati Msumbiji wakishangilia ushindi huo , hali ni tofauti kwa timu za Tanzania na Botswana ambazo hadi sasa hazijapata ushindi wowote katika michuano ya AFCON , Matokeo hayo yamezifanya timu hizo kubaki hazijapata ushindi toka walipoanza kushiriki michuano hiyo.
Michuano ya AFCON 2025 inaendelea kushika kasi huku kila timu ikipambana kuhakikisha inapata matokeo chanya, kinacho subiriwa ni kuona kama Tanzania na Botswana watafanikiwa kupata ushindi katika michezo Yao ya mwisho.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com



Post a Comment