Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) inayoendelea kufanyika nchini Morocco imeanza kwa kasi baada ya michezo minne ya kundi A na B kuchezwa, huku timu kadhaa zikianza kwa ushindi.
Katika Kundi A, timu ya Misri ilianza vyema mashindano baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Zimbabwe, Ushindi huo umeipa Misri pointi tatu na kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa kundi.
Mchezo mwingine wa kundi hilo ulizikutanisha Mali na Zambia, ambapo timu hizo ziligawana alama baada ya sare ya 1-1, kila upande ukionyesha ushindani.
Kwa upande wa Kundi B, Afrika Kusini ilipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Angola, Huku mwenyeji Morocco aliwafurahisha mashabiki wake baada ya kuifunga Comoros kwa mabao 2-0, ushindi uliothibitisha dhamira yao ya kutaka kutwaa ubingwa wakiwa nyumbani.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment