AFCON MOROCCO: MZUNGUKO WA PILI KUNDI A NA B EGYPT TIKETI MKONONI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Michezo ya mzunguko wa pili wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yanayoendelea nchini Morocco imechezwa kwa ushindani mkubwa katika kundi A na B, timu zimeendelea kupambana vikali kutafuta alama muhimu za kufuzu hatua inayofuata.

Katika Kundi A, matokeo yameendelea kuwa ya ushindani mkubwa huku kila timu ikionyesha nia ya kusonga mbele, hali hiyo imefanya msimamo wa kundi kubaki wazi kabla ya michezo ya mwisho ambapo wenyeji Morocco walitonashana nguvu ya 1-1 dhidi ya Mali , huku Comoro na Zambia wakigawana alama.

Kwa Kundi B, vigogo wa soka barani Afrika Misri wamejikatia tiketi kusonga mbele hatua inayofuata baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Bafana Bafana huku Angola na Zimbabwe wakitoshana nguvu ya 1-1.

Mzunguko wa pili ndipo mafuta na maji yanaanza kujitenga na katika hatua hii ndio baadhi ya timu zinaanza kupewa mkono wa kwaheri.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments