Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Timu ya taifa ya Morocco imetwaa ubingwa wa Mashindano ya Dunia ya Kiarabu baada ya kuibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Jordan katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Lusail, Qatar.
Katika mchezo huo uliovutia mashabiki Wengi , Morocco ilionesha morali na ushindani wa hali ya juu, ikirejea kwa nguvu baada ya kuwa nyuma na hatimaye kuibuka mabingwa wa dunia kwa nchi zaKiarabu.
Fainali hiyo ilishuhudiwa na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu akiwemo Emir wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad bin Khalifa Al Thani, pamoja na Mrithi wa Ufalme wa Jordan, Crown Prince Al-Hussein bin Abdullah II, hali iliyoipa uzito zaidi mechi hiyo ya kihistoria.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Gianni Infantino, alieleza kufurahishwa kwake na ubora wa mashindano hayo pamoja na hamasa kubwa ya mashabiki, akisisitiza kuwa mashindano hayo yameonesha mshikamano wa mataifa ya Kiarabu kupitia michezo.
Aidha, Shirikisho la Mpira wa Miguu la Qatar (QFA) lilipongezwa kwa maandalizi mazuri ya mashindano hayo yaliyounganisha mataifa ya Kiarabu na kutoa burudani ya kipekee kwa mashabiki wa soka duniani.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment