MOHAMED BAJABER NI NYOTA ISIYOZIMA KWENYE MIOYO YA WANASIMBA.

 

RASHID MSIRI

Mwanakwetu Sports.

Kila Mwanadamu kwenye maisha ya kila siku anapamba kuwa bora kwenye kile anachokifanya ili kuweza kuendana Kasi ya dunia pamoja na matamanio ya moyo wake.

Hakuna binadamu anayependa kupitia wakati mgumu kwenye maisha ila ni safari inayotujenga kuwa bora zaidii .

Haya ni maneno ambayo yatatokuwa yakijirudia mara kwa mara vichwani mwawanamichezo kutokana na Hali ngumu na vikwazo ambavyo wamekuwa wakipitia kwenye maisha yao ya kila siku, lakini hii ni tofauti kabisa na hadithi ya kufurahisha na iliyojaa huzuni kwa kiasi kwa mwanadinga Mohamed Bajaber .


Mohamed Bajabeerr ni Nani haswa?

Katika jiji la Nairobi nchini Kenya Jiji ambalo ni moja kati ya majiji machache duniani ambayo yana hifadhi ya taifa ya wanyamapori ndio eneo ambalo kijana huyu alizaliwa mwaka 2003, akitokea kwenye ukoo ambao una asili ya bara la Asia 🌏 katika falme za kiarabu, hata pale nchini Kenya ni moja ya familia kubwa inayojiweza kiuchumi.

Safari ya soka ya mwana ndinga huyu ilianza angalia akiwa kijana mdogo sana akicheza soka katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Nairobi huku akiwa bado kijana mdogo.

Uwezo wake wakusakata kabumbu uliwavutia watu wengi na vituo mbalimbali vya kukuzia vipaji vya mpira wa miguu wakiamini Mohamed Bajaber ni almasi iliyojificha Kwa taifa hilo.

Hatua hiyo ilizifanya taasisi mbalimbali za taaluma ya michezo kumuhitaji na hapa ndio safari yake ya kucheza soka la kulipwa ilianza kujengwa baada ya kujiunga na Starfield academy iliyopo parklands jijini Nairobi.

Hapa alipata misingi yote muhimu ya kiuchezaji anayopaswa kuwa nayo mwanasoka.

Kama waswahili wanavyosema kipaji hakijifichi, kauli hii inachukua nafasi kubwa kwa nyota Mohamed Bajaber kwani kutokana na uwezo wake wakusakata kabumbu ulivuvutia vilabu vingi barani ulaya wakiona ni dhahabu inayong’a zaidi sokoni.

Ndipo mnamo mwaka 2021, Mohamed Bajaber alifanikiwa kufunga safari yake ya kwanza kwenda kupambania ndoto yake ya kusakata kabumbu barani ulaya, klabu maarufu kutokea nchini Denmark ya midtyland na hapa ndio alipata fursa kubwa ya kujifunza mchezo wa soka kwani alikutana na wakufunzi bora wa soka kutokea barani ulaya lakini waswahili husema aliyenabahati habahatishi, kwani hakufanikiwa kusajiliwa timu ya wakubwa kutokana na majeraha yaliyokuwa yanamuandama.

Nyota wa mchezo wa masumbwi Muhammad Ali aliwahi kusema “ hushindwi unapodondoshwa bali pale unapokataa kuinuka” kauli hii inasadifu juu ya safari ya soka ya mchezaji Mohamed Bajaber kwani baada ya kushindwa kucheza soka la kulipwa barani ulaya hakukata tamaa bali aliendelea kupigania ndoto yake.

Mnamo mwaka 2022 aliamua kurejea nyumbani kwao nchini Kenya na kujiunga na klabu ya Nairobi city stars akitokea academy iliyomlea kabla ya kwenda kufanya majaribio nchini Denmark.

Akiwa Nairobi city, Mohamed Bajaber ndiyo alifanikiwa kucheza mchezo Wake wa kwanza wa ligi kuu nchini Kenya dhidi ya klabu maarufu kutokea nchini humo ya Tusker Mnamo 15 Mei 2022, ila ilimchukua michezo kadhaa kupita Hadi kufunga bao lake la kwanza Hadi pale alipofunga Goli dhidi ya klabu ya Wazito FC Mnamo Machi 16,2023.

Kutokana na kiwango bora alichokuwa nacho nyota huyo kilivutia vilabu vingi nchini humo na baada ya mkataba wake kumalizika msimu wa 2023-24 aliamua kujiunga na klabu ya Police Kenya Katika msimu wa 2024-25, baada ya kujiunga na klabu hiyo alifanya vizuri ikiwa alifanikiwa kufunga mabao 3 katika michezo mitatu ya awali ndani klabu hiyo.

Msimu wa 2025 hauwezi kusahaulika kichwani mwa mchezaji Mohamed Bajaber kwani ni moja ya msimu aliowahi kuwa na kiwango bora zaidii ambacho kilipelekea yeye kuitwa timu ya taifa ya Harambe Stars dhidi ya taifa ya Gambia ambapo alifunga goli katika mchezo huo ulioisha Kwa sare ya goli 3-3 .

Baada ya msimu wa mwaka 2024-25 kutamatika nyota huyo alikuwa katika rada ya vilabu vingi vya soka barani Afrika kutokana na kiwango.

Mnamo Agost 2025 Mohamed Bajaber alijiunga na miamba ya klabu bingwa Afrika Mashariki simba sports club huku kipindi hicho ikitajwa alikuwa katika kambi ya timu ya taifa ya Harambe Stars wakijianda na michuano ya CHAN.



Kutokana na ukubwa wa klabu ya soka ya simba mchezaji huyo aliamua kuondoka katika kambi ya timu ya taifa iliyokuwa chini ya kocha Ben Macath raia wa Afrika Kusini.

Muda uliwadia na viongozi wa simba waliamua kumsajili nyota huyo kama moja ya wachezaji wao wapya katika msimu wa mwaka 2025-26 .

Matarajio ya mashabiki wa simba yalikuwa makubwa kwa mchezaji huyo lakini alishidwa kuitumikia klabu hiyo kwa michezo ya mwanzoni kutokana na majeraha yaliyokuwa yanamuandama.

Nyota wa mchezo wa mpira wa kikapu Kobe Bryant aliwahi kusema “kila kitu hasi-presha, changamoto -ni fursa ya Mimi kuinuka” kauli hii inaweza pia kuchukua nafasi kubwa kwa nyota Mohamed Bajaber kwani baada ya majeraha ya muda mrefu aliweza kupambana na kurejea tena uwanjani na katika mchezo Wake wa kwanza wa ligi kuu nchini Tanzania iliweza kuisaidia klabu yake kupata ushindi wa Goli 3 kwa 0 na yeye akiwa mmoja wa wafungaji katika mchezo huo akitokea benchi.

 Katika maisha ya soka siku zote bingwa hafafanuliwi na ushindi, bali jinsi anavyoinuka baada ya kuanguka , licha ya safari ngumu aliyopitia mchezaji Mohamed Bajaber lakini hajawahii kukata tamaa na kuacha kujaribu .

Safari ya soka ya nyota Mohamed Bajaber imejaa mengi ya kusimulia ila ni sawa na kitabu ambacho mtunzi wake bado hajamaliza kukiandika.


rashidmsiri@gmail.com

0754645826




0/Post a Comment/Comments