Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Liguu ya NBC iliendelea hapo Jana ambapo klabu ya Simba ilijikuta ikipokea kichapo Cha 2-0 dhidi ya matajili wa Chamanzi Azam fc kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa.
Mabao ya wana lambalamba yaliwekwa kimiani na Kitambala 83' na Iddy Nado 89' , kipigo hiki kinakuwa ni mfululizo wa matokeo mabovu wanayokumbana nayo klabu ya Simba ikiwa ni mchezo wa tatu wanapoteza ndani ya miezi miwili jambo ambalo linatia wasiwasi kuhusu mwenendo wa timu.
CHANGAMOTO MATUMIZI YA NAFASI
Licha ya kumuachisha kazi aliyekuwa meneja wa klabu Pantev lakini tatizo hali jatibika bado wachezaji wa Simba hawako makini kwenye umaliziaji wa nafasi wanazo tumia , Joshua Mutale na Mukwala walidhihirisha hilo baada ya kushindwa kukwamisha mpira kimiani walipopata nafasi za wazi.
NAFASI YA MUTALE
Kipindi Cha kwanza Mutale alipata nafasi ya kukwamisha mpira kimiani wakati ambao Golikipa wa Azam Zuberi Foba alitoka langoni na kuukosa mpira huku akiacha lango wazi lakini Mutale akishindwa kukwamisha mpira Kimiani na badala yake mpira ukapaa juu la lango.
NAFASI YA MUKWALA
Baada ya shambulizi la hatari lililofanywa na Elie Mpanzu kwa kupiga shuti lililo gonga mwamba wa chini na kurudi ukimkuta Mukwala kwenye eneo sahihi kilikuwa ni kitendo Cha kuusukumiza mpira wavuni lakini aliupaisha mpira juu ya lango na kuukosa nafasi ya kuwapa Simba bao.
MASHABIKI WAIMBA MANGUNGU AONDOKE
Baada ya mchezo huo mashabiki wa Simba walionyesha kuwa na hasira kuhusu mwenendo mbovu wa timu Yao ambapo walisikika wakiiimba " Hatumtaki Mangungu" wakishinikiza kujiuzuru kwa mwenyekiti wa timu hiyo.
Sio muda sahihi kwa klabu kubwa kama Simba kuanza lawama kwa viongozi wao wakati tatizo lilnalo wafanya wasipate matokeo linaonekana, " wachezaji kutotumia nafasi" , badala yake wadau na viongozi waangalie namna sahihi ya kuinusuru timu Yao kutoka kwenye Hali mbaya wanayopitia hivi sasa.
NINI KIFANYIKE
Viongozi, benchi la ufundi na wachezaji wakae kwa pamoja na kuzungumza kwa pamoja ili kubaini ni changamoto gani wanazo wachezaji wao Hadi wanashindwa kutumia nafasi za wazi wanazozipata na kusababisha matokeo mabovu na sio kunyosheana vidole kwenye kipindi kigumu kama hiki , Simba ni timu kubwaa wanahitaji kutatua matatizo kikubwa.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment