Timothy Lugembe
Mwanakwetusports.
Klabu ya Liverpool imegonga vichwa vya wanasoka baada ya kocha wake, Arne Slot, kueleza kuwa nyota wa timu hiyo, Mohamed Salah, anapaswa kuanza mchakato wa kutatua mvutano uliosababisha kukosa mchezo wao dhidi ya Inter Milan.
Slot alizungumza baada ya ushindi wao dhidi ya Inter, akibainisha kuwa suala la kutengana kati ya mchezaji na benchi la ufundi linaweza kutatulika kwa urahisi endapo wote watakuwa tayari kukubali makosa, hata hivyo, kocha huyo alionyesha wazi kuwa anasubiri hatua ya kwanza kutoka kwa Salah ili kurejesha hali ya kawaida ndani ya kikosi.
Kauli hiyo imeongeza maswali kuhusu chanzo cha sintofahamu hiyo, huku mashabiki wakitaka kufahamu iwapo kuna mgongano wa kitabia au tofauti za kiufundi kati ya mchezaji huyo muhimu na benchi la ufundi, Slot alieleza kuwa mazungumzo bado yanawezekana, lakini uamuzi wa kuanza suluhu unapaswa kuanzia upande wa Salah.
Tukio la kutengwa kwa Salah kwenye mchezo wa dhidi ya Inter lilizua hofu kwa wapenzi wa Liverpool, kwani mchezaji huyo amekuwa mhimili mkubwa wa timu kwa miaka kadhaa hadi sasa, bado haijafahamika ni lini hali itarejea kuwa shwari, lakini ishara zinaonyesha kuwa suluhu inaweza kupatikana iwapo Salah ataonyesha utayari wa kurejea mezani.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment