Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Dhoruba ya matokeo mabovu imeikumba klabu ya Simba kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika, kitu ambacho ni kinyume na matarajio ya Wengi hatua iliyomfanya meneja huyo kufungashiwa virago vyake klabuni hapo.
Klabu ya Simba ipo kundi D pamoja na timu za Esperance, Petro Atletico na Stade Malien ambapo katika michezo miwili waliyocheza wamepoteza yote. Mchezo wa kwanza walifungwa 1-0 wakiwa nyumbani dhidi ya Petro Atletico, huku mchezo wa pili walikubali kichapo Cha 2-1 na Stade Malien ugenini, matokeo hayo yanawafanya Simba kuburuza mkia katika kundi hilo.
Kabla ya kuanza michezo Simba walipewa nafasi kubwa ya kuongoza kundi au kushika nafasi ya pili kutokana na uwezo wao wa kuvuna alama uwanja wa nyumbani , pia kwa kuzingatia viwango vya ubora wa vilabu Afrika, lakini meza imepinduka imekuwa tofauti na matarajio.
SABABU ZA MATOKEO MABOVU
Klabu ina waachezaji Wazuri wenye uzoefu lakini changamoto imekuja kwenye utumiaji wa nafasi, katika hatua ya makundi Kila timu inatakiwa kuwa makini kwenye utumiaji wa nafasi ili kufunga mabao na kuvuna alama zitakazo wasogeza mbele, lakini kwa Simba imekuwa tofauti wamekuwa wakitengeneza nafasi za wazi lakini kukwamisha mpira wavuni imekuwa tatizo.
Mchezo wa pili dhidi ya Stade Malien Simba walitengeneza nafasi toka kipindi Cha kwanza lakini ufanisi wa umaliziaji uliKosekana na badala yake wapinzani walipopata nafasi chache walizigeuza kuwa mabao na kuwaacha Simba wakiambilia kichapo.
KWANINI MENEJA ASILAUMIWE?
Meneja wa klabu hiyo Pantev hatakiwi kupewa lawama hata kidogo sababu kikosi anapanga vizuri ila tatizo limekuwa kwa wachezaji wenyewe kushindwa kutumia nafasi wadau wanaweza kujiuliza kupitia mchezo wa kwanza kwanini hakuanza na washambuliaji halisia? huenda ikawa sababu ya klabu kuukosa matokeo, sio kweli lengo la kocha lilikuwa ni kumiliki mpira na kutengeneza nafasi, alifanikiwa kwenye kutengeneza nafasi lakini wachezaji walimuangusha, kwanini alaumiwe?
Baada ya mchezo dhidi ya stade Malein Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Neo Maema, amesema kuwa sababu ya timu hiyo kupoteza mechi mbili mfululizo za CAF Champions League ni makosa yao wenyewe.
Maema amewapongeza mashabiki kwa sapoti kubwa wanayoitoa, lakini amekiri kuwa wachezaji hawajatekeleza majukumu yao ipasavyo uwanjani, ikiwemo kushindwa kutumia nafasi wanazopata katika mechi.
Ameongeza kuwa benchi la ufundi huwapa mbinu na maandalizi mazuri kila siku, lakini bado wameshindwa kuyatekeleza ipasavyo ndani ya dimba.
Hivyo kutokana na kauli ya Maema klabu ingezidi kumpatia muda Meneja huyo ili azidi kuzoe kikosi kuliko maamuzi waliyofanya huenda yaka igharimu zaidi kutokana na Kila kocha na falsafa zake je, izo falsafa za kocha mpya zitachukua muda gani kuwaingia wachezaji?
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.




Post a Comment