MECKY MAXIME KUIONGOZA PURPLE NATION

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports

Klabu ya Mbeya City imeanza ukurasa mpya baada ya kutangaza rasmi kumkabidhi Mecky Maxime majukumu ya Kocha Mkuu, kufuatia uamuzi wa kuachana na benchi lote la ufundi lililokuwa likiiongoza timu hiyo hadi mwishoni mwa mwezi Novemba.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo Novemba 30, 2025 ilithibitisha kusitishwa kwa mkataba wa aliyekuwa Kocha Mkuu Malale Hamsini pamoja na makubaliano ya kuvunja mikataba ya aliyekuwa kocha msaidizi Mussa Rashid, kocha wa magolikipa Wilbert Mweta na daktari wa timu Dkt. Hashraf Mapunda, hatua hiyo ilielezwa kuchochewa na kutoridhishwa kwa uongozi na mwenendo wa timu kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League), ikiwemo matokeo duni yaliyowafanya kushuka kwenye nafasi za hatari.

Baada ya mabadiliko hayo, Mbeya City imeamua kumsajili kocha Mecky Maxime kama Kocha Mkuu mpya kwa lengo la kuibadilisha sura ya timu na kurejesha ushindani wanaoutarajia kutoka kwa Purple nation

Maxme, anayefahamika kwa mbinu za soka za kisasa na uwezo wa kuwatengeneza wachezaji vijana, anatarajiwa kuleta mabadiliko ya haraka ili kuokoa msimu wa klabu hiyo inayohitaji kupanda kwenye nafasi salama kwenye msimamo wa ligi.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments