MBEYA CITY YAACHANA NA BENCHI LAKE LA UFUNDI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Mbeya City imefanya maamuzi ya kuachana na benchi lake la ufundi kufuatia mwenendo usioridhisha kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwemo kipigo cha 1-0 walichokipata nyumbani dhidi ya Namungo FC.

Katika taarifa ambayo klabu imetoa Novemba 30, 2025, uongozi wa Mbeya City umetangaza kuachana na Kocha Mkuu Malale Hamsini Uamuzi huo pia umeambatana na kusitishwa kwa mikataba ya Kocha Msaidizi Mussa Rashid, Kocha wa Magolikipa Wilbert Mweta pamoja na Daktari wa timu, Hashraf Mapunda.

Chanzo cha hatua hiyo kimeelezwa kuwa ni kutoridhishwa kwa uongozi na namna timu ilivyokuwa ikifanya katika michezo ya ligi, matokeo yaliyozidi kudorora na kumalizia kwa kichapo cha nyumbani ambacho kimeonekana kuwa nusura ya mwisho kwa benchi hilo la ufundi.

Mbeya city inawa takia Kila lakheri kwenye majukumu Yao mengine.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments