Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Rekodi mbili kubwa zilizokuwa zikishikiliwa na nyota wa soka duniani, Cristiano Ronaldo, zimefutwa rasmi baada ya washambuliaji wawili mahiri, Kylian Mbappe na Erling Haaland, kuandika historia mpya katika uga wa ulaya.
Mbappe aliingia vitabuni jana baada ya kuivunja rekodi ya Ronaldo ya ufungaji bora wa kalenda akiwa na klabu ya Real Madrid, Mshambuliaji huyo wa Ufaransa alifikisha mabao 59 ndani ya mwaka mmoja baada ya Jana kufunga bao dhidi ya Sevila akifikia idadi ya mabao ambayo Ronaldo aliyafunga mwaka 2013 alipokuwa klabuni hapo.
Kwa upande mwingine, Haaland naye hakubaki nyuma, alivunja rekodi ya Ronaldo ya kufunga mabao mengi katika michuano ya Premier League(ligi kuu Uingereza) , Haaland alifikisha jumla ya mabao 104, akipita rekodi ya awali ya Ronaldo ya mabao 103.
Tukio hilo limezua mjadala mkubwa miongoni mwa wachambuzi na mashabiki wa soka, wengi wakitafsiri kuvunjwa kwa rekodi hizo kama ishara ya kupanda kwa kizazi kipya cha washambuliaji wanaochukua nafasi ya vigogo wa zamani.
Hata hivyo, jina la Ronaldo linaendelea kubaki katika mioyo ya wengi kama mmoja wa wachezaji wakubwa zaidi kuwahi kutokea, licha ya rekodi zake kuvunjwa Mbappe na Haaland sasa wanaandika historia yao, wakithibitisha kuwa soka la kisasa limeingia sura mpya yenye ushindani mkubwa.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment